March 16, 2019


Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Azam FC wamalizana na straika wake Donald Ngoma kwa kuongeza mkataba wa miaka miwili, taarifa za ndani kutoka kwa matajiri hao zinaeleza imekuwa ni ngumu kumalizana na Mzambia, Obrey Chirwa.

Taarifa imeeleza kuwa Chirwa ambaye anamaliza mkataba wake wa miezi 6 na Azam mwishoni mwa msimu huu amegoma kuongeza mwingine baada ya kutoafikia kiasi cha fedha ambacho Azam wamekiweka mezani.

Wakati ikielezwa Chirwa amegoma, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, wameanza mazungumzo na mchezaji huyo pamoja na klabu ili kuchukua saini yake.

Kiasi cha dau la milioni 85 kinaweza kumsainisha Chirwa mkataba wa miaka miwili Simba ambalo mchezaji mwenyewe ameonekana kulipokea.

Afisa Mtendaji wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat' amesema walikaa na Chirwa kuzungumza lakini ameonesha hana nia ya kuendelea na Azam kutokana na dau walilomtajia.

"Chirwa alisaini mkataba wa miezi sita pekee na tumekuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mwingine, lolote linaweza kutokea.

"Kuhusu kwenda Simba si jambo la kushutua maana ndiyo maisha ya mpira na wachezaji kwa ujumla, mchezaji anaangalia wapi pana maslahi mazuri."


7 COMMENTS:

  1. Yani nyie ni kucopy na kupaste tu kila wanachopublish mwanaspoti

    ReplyDelete
  2. Atakaelisajili hill yeboyebo alipeleke nyumbani kwake sio Simba Sports Club

    ReplyDelete
  3. Chirwa yupo vizuri hakuna ubishi na timu kama ya Simba itamfanya awe mzuri zaidi. Simba hawana haja ya kulaza damu katika usajili wa Chirwa kwani ni miongoni mwa wachezaji wapambanaji haswa anapokuwa kwenye timu inayomtimizia mahitaji yake.

    ReplyDelete
  4. Dah,simba tafuteni wachezaji wa maana basi!

    Namna hii kila ikienda nje unapigwa 5

    ReplyDelete
  5. Dah,simba tafuteni wachezaji wa maana basi!

    Namna hii kila ikienda nje unapigwa 5

    ReplyDelete
  6. Binafsi siwezi kuzungumza chochote maana swala la usajili liko kwa mwalimu yeye ana jicho LA kipekee!

    ReplyDelete
  7. Imefungwa na Lipuli bado unazungumza.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic