MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amesema anatambua umuhimu wa mashabiki na ameguswa na kilio cha mtoto Rackeem hivyo anaamini watafanya vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya AS Vita utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa.
Mtoto Rackheem wa Tanga alizua gumzo baada ya mzazi wake kumrekodi video akilia baada ya kusikia Simba imefungwa mabao 2-0 na JS Saoura huku mshambuliaji wake anayempenda Kagere akishindwa kufunga bao.
Kagere amesema kuwa anatambua thamani ya mashabiki wake na umuhimu wa michezo ya Ligi ya Mabingwa hivyo wachezaji kwa ujumla wanajiaanda kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya AS Vita utakaochezwa Jumamosi.
"Maumivu ya mashabiki wetu nayatambua na ninashukuru kwa kuwa wengi wapo pamoja nasi na wanatuombea dua hivyo tutapambana kupata matokeo mchezo wetu wa mwisho hakuna kingine tunahitaji matokeo.
"Mtoto aliyelia juu yangu inaonesha ni namna gani anajali ila sina mashaka kwa kuwa najua atakuja Uwanja wa Taifa nitapata pia muda wa kupiga naye picha sina tatizo na mashabiki wangu," amesema Kagere.
0 COMMENTS:
Post a Comment