BAADA ya wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Ramadhan Kabwili pamoja na beki Abdalah Shaibu 'Ninja' kusema kuwa nahodha msaidizi Juma Abdul ni mtu wa 'fiks' nahodha amewatolea uvivu kwa kuwajibu.
Ninja alisema kuwa "Abdul ana maneno mengi tukiwa kambini, halafu muongo kweli hali inayofanya akiwa kambini wachezaji kucheka wakimuona,".
Abdul amesema kuwa amewasikia wachezaji wenzake wakisema kwamba yeye ni muongo jambo ambalo limemfanya afurahi kwani hajawahi kuwaongopea.
"Unajua wale bado ni chipukizi na damu inachemka sasa wakikutana wenyewe kupiga stori zao wanaanza kuchanganya mambo, mimi naishi nao poa tu kambini bila shida yoyote.
"Naona wanazingua tu kuhusu hilo hakuna ukweli wowote, tunapiga stori za kawaida na tunapendana kwa kuwa sisi ni familia," amesema Abdul.
Abdul msimu huu hajawa na nafasi kubwa ndani ya kikosi cha kwanza kutokana na kusumbuliwa na majeruhi kwa sasa nafasi yake imebebwa na kinda Paul Godfrey.
يلا شوت بث مباشر
ReplyDeleteيلا شوت مباريات اليوم
تركيب دش
صيانة الدش
تركيب الدش
مباريات اليوم
بث مباشر
كورةvib