March 13, 2019


KIKOSI cha Simba ambacho kwa sasa kampeni yake ni Do or Die, bongo kimecheza michezo 20 nafasi ya tatu na kimekusanya pointi 51 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 67 Ligi Kuu Bara.

Michezo yake ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Taifa hajapoteza hata mchezo mmoja kuanzia ile ya awali mpaka makundi.

Alianza kushinda dhidi ya Mbabane mabao 4-1, Nkana FC 3-1, JS Saoura 3-0 na Al Ahly 1-0.

Mpinzani wake AS Vita kwenye Ligi ya Congo kwenye michezo 23 imeshinda michezo 20 na kujikusanyia pointi 62.

Mchezo wao uliopita waliwanyoosha Al Ahly bao 1-0 hali iliyowafanya wafikishe pointi saba sawa na Al Ahly wakiwa nafasi ya tatu.

Jumamosi watamenyana na Simba mchezo wa marudio wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 5-0 waliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza.

Kila timu inahitaji ushindi ili kupenya hatua ya robo fainali hivyo mashabiki wa Simba wajitokeze kutoa sapoti kwa timu kwa manufaa ya klabu na taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic