WASHAMBULIAJI wa Azam FC, ambao walikuwa pamoja kwenye kikosi cha Yanga wameanza kunoga ndani ya kikosi hicho baada ya kuendelea kujaza akaunti yao ya mabao kwenye ligi.
Azam FC ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha Idd Cheche baada ya kucheza michezo 26 haikuwa na mfungaji ambaye amefikisha mabao saba ila kwa sasa tayari wameshavunja rekodi hiyo.
Donald Ngoma kwenye ushindi wa mabao 6-1 mbele ya JKT Tanzania alipachika mabao 2 na kufanya akaunti yake ijae mabao kutoka mabao matano mpaka kufikia mabao 7 sawa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
Kwa upande wa Chirwa yeye bado anakuja taratibu kwani yeye alikuwa ana bao moja tu na bao alilofunga dhidi ya JKT Tanzania linamfanya awe na mabao 2 na assit yake moja mguuni.
Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza michezo 27 imejikusanyia pointi 56 kibindoni kwa sasa huku kinara ni Yanga mwenye pointi 67.
0 COMMENTS:
Post a Comment