March 3, 2019


KIKOSI cha Simba kimekuwa na moto wa aina yake kwani tangu waanze kumega viporo vyao msimu huu kasi yao inatisha hawajapoteza hata mchezo mmoja wao wanajipigia tu.

Rekodi zinaonyesha ni mchezo mmoja walishinda kwa idadi ndogo ya mabao kuliko michezo yote ambayo wamecheza  na wameruhusu mabao mawili huku wakifunga mabao 13.

Rekodi zao zipo namna hii kwa mechi tano za viporo ambazo Simba wamecheza na kipa Aishi Manula kukaa langoni:-

Simba 3-0 Mwadui, Uwanja wa Tiafa, Yanga 0-1 Simba, Uwanja wa Taifa, Lyon 0-3 Simba Sheikh Amri Abeid, Azam 1-3 Simba, Uwanja wa Taifa na Lipuli 1-3 Simba Uwanja wa Samora.

Beki wa Simba, Pascal Wawa amesema kuwa mazoezi wanayopewa na mbelgiji Patrick Aussems na ushirikiano ndani ya timu unawabeba.

"Kazi sio nyepesi kwani ipo wazi kila timu inaonyesha ushindani kutafuta pointi tatu, ni jambo la kushukuru kwa kuwa tunapata matokeo," amesema Wawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic