March 3, 2019


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa leo ni mwendo wa kichapo tu kwa wapinzani wao Prisons katika mchezo wao wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Singida kwa msimu huu imekuwa ikisuasua kupata matokeo, ipo chini ya kocha msaidizi Fred Minziro baada ya kocha mkuu Dragan Popadic kupata adhabu ya kufungiwa michezo mitatu kwa kumzonga mwamuzi kwenye mchezo wao dhidi ya Ndanda FC.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema wanatambua ugumu wa ligi ulivyo ila ni wakati wao kutumia Uwanja wa nyumbani kupata matokeo.

"Tumepoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City sasa hatuna kingine zaidi ya kuwanyoosha wapinzani wetu Prisons, mashabiki wajitokeze kuipa sapoti timu, kwa pamoja tunaweza," amesema Katemana.

Singida United imecheza michezo 26 imeshinda 7 imepoteza 11 huku ikiwa na sare ya michezo 8 na kibindoni ina pointi 29.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic