March 1, 2019

Kikosi cha klabu ya Simba kimeondoka mjini Singida asubuhi ya leo kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mechi na Stand United Jumapili hii.


Simba wameondoka Singida walipoweka mapumziko ya muda mfupi kisha kuendelea na mazoezi jana kwenye Uwanja wa Namfua.

Wakati Simba wakiwa njiani, wapinzani wao Stand United wameweka kambi Bariadi, Simiyu tayari kwa kuandaa dawa maalum ya kuwamaliza Simba.

Stand wametamba kuhakikisha wanaimaliza Simba ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 48.

Imeelezwa mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu zaidi mkoani humo haswa kutokana na namna Simba ilivyosheheni wachezaji wengi walio na majina makubwa.

1 COMMENTS:

  1. Mpila ni dakika 90 hivo basi kilammoja atashuhudia kwa macho yake mawili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic