UONGOZI wa KMC umesema kuwa kesho wataonyesha namna ya ubora wa kikosi chao kilivyo kwa kikosi cha wafanyabiashara kutoka Mara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
KMC kesho wataikaribisha Biashara United kwenye mchezo wa ligi kuu ikiwa ni mzunguko wa pili.
Ofisa Habari wa KMC, Anuwari Binde amesema wanatambua ushindani uliopo kwenye ligi na namna kila timu inavyotafuta matokeo ila wao wataonyesha utofauti.
"Kikosi kipo sawa na tupo tayari kwa mapambano, tutaingia uwanjani tukiamini kwamba tunacheza na timu ngumu, ila kikubwa tutakachofanya ni kutumia vema Uwanja wa nyumbani," amesema Binde.
KMC imecheza michezo 27 ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 40, ni kinara kwa timu zote ambazo zimepanda daraja msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment