KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa ushindi wake mbele ya kikosi cha Mtibwa Sugar umewapa nguvu mpya ya kupambana zaidi.
Kagera Sugar waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wao wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera hivi karibuni.
Maxime amesema kuwa juhudi za wachezaji pamoja na mbinu kali alizowapa wachezaji wake ziliwasaidia kupata matokeo.
"Tuliwasoma vizuri wapinzani wetu namna walivyo na kasi tukajua namna bora ya kuwazuia, kwa sasa ligi inavyokwenda kila mmoja ni lazima apambane kupata matokeo na hicho ndicho tulichokifanya kwa wapinzani wetu.
"Kwa sasa hesabu zetu ni kuona tunapata matokeo kwenye michezo yetu yote iliyobaki na pia tunajiaanda kwa ajili ya kucheza na Azam FC kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho utakaochezwa mwezi huu," amesema Maxime.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 29 ikiwa na pointi zake 36 huku Mtibwa Sugar wakiwa nafasi ya 6 na pointi 41 baada ya kucheza michezo 29.
0 COMMENTS:
Post a Comment