March 19, 2019


KIKOSI cha Biashara United kilicho chini ya kocha mkuu, Amri Said kimezidi kuididimiza timu ya African Lyon baada ya kuwafunga bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa Uwanja wa Karume mkoani Musoma.

Mpaka sasa Lyon katika michezo 31 waliyocheza wameshinda michezo minne pekee huku wakipoteza michezo 14 na kupata sare michezo sita pekee.

Lyon wanaburuza mkia kwenye msimamo wakiwa na pointi 22 pekee licha ya kuwa timu ambayo imecheza michezo mingi kwenye ligi.

Kocha Mkuu Said amesema kuwa anatambua wachezaji wake wana jituma ila bado kinaochoimaliza timu yake ni ukata na kusistiza mashabiki wasichoke kuisaidia timu yao.

"Tunashinda na tutaendelea kushinda ila kikubwa ni ukata tu kwa sasa ambao unatusumbua mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti na tunaamini tutafanya vizuri michezo yetu ijayo," amesema Said.

Biashara United imecheza michezo 29 ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi kuu bara baada ya kujikusanyia pointi 30 kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic