KUTOKANA na mchezaji wa timu ya Alliance FC, Juma Nyangi kuonekana akifanya kitendo kisicho cha kinidhamu kwa mchezaji wa tImu ya Yanga, Gadiel Michael kamati ya nidhamu imeamua kumpa adhabu ili kuwa funzo kwake.
kitendo cha Nyangi kumpapasa makalio mchezaji wa Yanga kilinaswa na kamera za Azam TV kwenye mchezo huo ambao ulichezwa Uwanja wa CCM Kirumba na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu wa klabu ya Alliance, Yusufu Budodi amesema kamati iliamua kufanya kikao kumjadili mchezaji huyo na walimpa nafasi ya kujitetea kabla ya kutoa maamuzi.
"Tumemsikiliza mchezaji wetu na tukapitia kanununi, tukafanya maamuzi ya kumpa adhabu ambayo itakuwa ni funzo kwa wengine ambapo kamati imeamua kumkata mshahara wa mwezi mmoja na kumpa onyo kali.
"Tunaamini itakuwa funzo kwake na tunaomba radhi kwa wadau wa mpira kutokana na kosa la mchezaji wetu, tumeanza kufanya hivyo na hatukuamua kumfungia mechi baada ya kuona ni kosa lake la kwanza," amesema Budodi.
Ninja vipi uchafu aliyofanya coastal union?au ndio wanasubiri ligi iishe
ReplyDeleteSioni ajabu.Ngoma mpaka ligi iliisha hakuna hatua zilizochukuliwa.
ReplyDeleteNi aibu na kashfa klabu kuchukua hatua wakati TFF ipo kimya!
ReplyDeleteImekuwa kawaida sasa utovu wa nidhamu kutokuchuliwa hatua .
Sheria si msumeno
ReplyDeleteHIKI NI KIINI MACHO TUNATAKA ADHABU ITOKE TFF, KLABU MMEFANYA VIZURI KUMUADHIBU LAKINI HAITOSHI TFF LAZIMA MCHUKUE HATUA KALI ZAIDI YA KUMFUNGIA NA KUMPIGA FAINI TUNA MIFANO YA JUMA NYOSSO NA WENGINE WALIFANYA UPUUZI HUOHUO, HUYU NAYE LAZIMA AFUNGIWE
ReplyDelete