KESI YA WAMBURA YAFANYIWA TENA MAAMUZI MENGINE
KESI inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura imeahirishwa kutokana na upelelezi kutokamilika.
Wakili wa serikali, Wonkey Simon aliiambia mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika ila umefikia katika hatua nzuri kwa sasa.
Wambura anakabiliwa na mashitaka 17 ikiwemo shitaka la utakatishaji fedha na kughushi akiwa mfanyakazi wa TFF.
Kesi hiyo inasimamiwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kelvin Mhina.
Hata hivyo, katika kesi hiyo mawakili upande wa mshitakiwa wakiongozwa na Majura Magafu hawakuwezi kutokea kwenye kesi hiyo na sababu hazikuwekwa wazi. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Machi 28, mwaka huu.
Wambura anaendelea kukaa mahabusu kutokana na kesi yake kutokuwa na dhamana.
0 COMMENTS:
Post a Comment