KIFAA KIMOJA CHONGEZWA YANGA
Baada ya kutoonekana dimbani kwa mechi kadhaa, kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, amejumuishwa katika wachezaji watakaocheza dhidi ya Alliance FC.
Kamusoko ambaye alikuwa majeruhi amejiunga na wachezaji wenzake kuelekea mechi ya kesho na Alliance ambayo itapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kurejea kwa Kamusoko inaweza kuwa chachu ya nafasi ya kiungo kwa Yanga kuongeza makali haswa katika upikaji wa mipira kuelekea eneo la ushambuliaji.
Wakati huo Yanga imeendelea na mazoezi jana na leo itafanya ya mwisho kabla ya kukipiga na Alliance.
Kuelekea mechi hiyo, Yanga mpaka sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 61 dhidi ya Azam yenye 50 na Simba ikiwa na 48.
0 COMMENTS:
Post a Comment