March 1, 2019


Hauwezi amini lakini ndiyo maneno ya Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, ameibuka na kusema kuwa timu yake ndiyo inayofuatiliwa zaidi kwa sasa.

Bwire ambaye ni msemaji asiyeishiwa na maneno, ameeleza namna ya soka ambalo Ruvu Shooting inacheza inasababisha timu yake kufuatiliwa kuliko kawaida.

Amefunguka kuwa Ruvu inacheza soka la kisasa ambalo timu nyingine zinashindwa kuhimili aina ya mchezo huo wa soka na kuifanya timu izidi kuwa na wadau wengi.

"Hakuna timu ambayo inafuatiliwa zaidi kama Ruvu Shooting kwa sasa, tuko vizuri na tunapiga soka la kisasa kabisa na ndiyo maana tunazungumziwa kila iitwapo leo" alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic