Baadhi ya wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga wamehoji kuachwa kwa Nahodha wao, Ibrahim Ajib katika kikosi cha Taifa Stars kilichotangazwa na Kocha Emmanuel Amunike.
Kikosi hicho kimetangazwa jana kwa ajili ya kuanza rasmi maandalizi ya mechi ya kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda itakayopigwa Machi 24 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya kukosekana kwa Ajib, mashabiki hao wameeleza kushangazwa na maamuzi ya Kocha Amunike, huku wengine wakieleza pengine kuna namna kati yake na mchezaji kwasababu hajawahi kumuita tangu apewe timu hiyo.
Wakizungumza nasi huku wakitaka majina yao kutowekwa hadharani, wamemshauri Kocha huyo kutokariri kikosi na badala yake mtu kama Ajib wakisema alipasw aitwe wakiamini ndiye nguzo muhimu kwa Yanga.
Wamemzungumzia Ajib kuisaidia Yanga mpaka hapo ilipofikia katika kutengeneza mabao halikadhalika kupachika nyavuni.
Ukiachana na Ajib, baadhi yao pia wamemtaja beki Abdi Banda ambaye amekuwa akisakata kabumbu lake Baroka FC ya Afrika Kusini kutojumuishwa katika kikosi kuwa naye alipaswa kuitwa.








AJIB, TSHABALALA, NA KIMENYA? WANASTAHILI KABISA KUCHEZEA TIMU YA TAIFA. KWANI TIMU HII YENU PEKE YENU? MBONA MNAPENDELEA? WACHEZAJI WANAJITUMA KWENYE VILABU NYINYI MNABAGUA DHAMBI KUBWA KWA MUNGU HIVYOHIVYO MLIWAKATAA WACHEZAJI WA SIMBA ETI KISA WAMECHELEWA KURIPOTI KWA USIKU MMOJA TU. AMUNIKEEEE
ReplyDeleteNdiyo maana Timu haifikagi mbali sababu ya teuzi za kuangaliana sura Na sio uwezo wa mchezaji
ReplyDeleteAmunike sio kocha kwanza hajiamini na kazi yake. Usishangae ukaja ukaona anaingia kwenye mechi na Uganda na mfumo wa kujilinda wakati Taifa stars wanatakiwa kushinda kwenye mechi hiyo.kocha gani anaeshikwa sikio katika uteuzi wa kikosi chake.kamwe Amunike hawezi kuwa na maamuzi ya kubalanzi idadi ya wachezaji wanaotakiwa kujiunga Taifa stars kutoka Simba na Yanga. Utaona kabisa katika uteuzi wa kikosi chake kilichoangaliwa ni kubalanzi idadi ya wachezaji kutoka timu husika na sio uwezo wa wachezaji kutoka timu husika yaani ni siasa za kijinga kabisa kwenye mpira.
ReplyDeleteSwala la Ajibu limechukua mjadala mkubwa sana katika mitandao ya kijamii ila kitu cha kujiuliza ni kwamba Kocha AMEANGALIA KITU GANI KATIKA UTEUZI WA WACHEZAJI HASWA KWA NAFASI AMBAYO ANACHEZA IBRAHIMU AJIBU KISHA KUTOA COMENT KULINGANA NA WACHEZAJI AMBAO ANACHEZA NAO NAMBA MOJA , JE AKUSTAHILI KWA SABABU .MFANO KWANINI KAMUACHA AJIBU KAMCHUKUA SAMATA AMBAYE ALIKUWA KATIKA KIWANGO CHA CHINI HAPO TUNAWEZA KUPATA TUNACHOKITAKA LAKIN AJIBU HUYO AMEONEKANA KATIKA MECHI ZA HIVI KARIBUNI KUTOKEA SABU NA KAMA AKIANZA AMALIZI DAKIKA 90 NA WAKATI AKITOLEWA TIMU INAKUWA HAIJAPATA MATOKEO HIVYO INAONYESHA KUWA HAKUWA NA MSAADA KAMILIFU KWA TIMU YAKE ...... LAKINI TUKIANGALIA KUPIGA CHENGA AU KUPENDWA NA WASHABIKI WENGI WA MPIRA TANZANIA NA SIO KUTENGENEZA KIKOSI CHENYE UBORA NA USHINDANI SAWA YEYOTE ANAWEZA KUITWA KWA LENGO AKACHEZE NA SIO KULETA USHINDI KWA TAIFA.
ReplyDeleteSio Ajibu peke yake? Jiulize waganda wamewaita wachezaji wangapi? CONGO DRC wamewaita wachezaji wangapi? Kuna khasani Dilunga,salum Abubakari sure boy hawa wote wapo vizuri zaidi kuliko baadhi ya wachezaji walioitwa na Kocha wa stars. Kocha angeita hata wachezaji thelathini 30 au zaidi akawafanyia mchujo kuna tatizo gani? Waganda wanaoweka kambi yao ugenini wamewaita wachezaji wengi zaidi kuliko sisi timu yetu itakayokuwepo hapa nyumbani.
ReplyDelete