March 9, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hesabu kubwa leo ni kuona wanapata pointi mbele ya wapinzani wao JS Saoura kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa nchini Algeria.

Simba wana kibarua kizito leo kutokana na kuwa na matokeo mabaya ugenini hasa baada ya kutinga hatua ya makundi kwani kwenye mechi mbili ambazo walitoka zote walifungwa, walianza mbele ya AS Vita wakafungwa 5-0 kisha mbele ya Al Ahly walipigwa 5-0.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua ugumu wa mechi ila watapambana kupata matokeo.

"Ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila hesabu kubwa ni kuona tunapata matokeo ili tuweze kusonga mbele kwani kila mmoja anahitaji kwenda hatua ya robo fainali, mashabiki msisahau kutuombea," amesema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic