March 24, 2019


BAADA ya kuwa nje tangu Novemba mwaka jana, beki wa Simba, Shomary Kapombe sasa yuko fi ti na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki ijayo.

Kapombe aliumia kifundo cha mguu kwenye kambi ya Taifa Stars iliyowekwa nchini Afrika Kusini ambako walikuwa wakijiandaa na mechi dhidi ya Lesotho, beki huyo alifanyiwa upasuaji.

Kwa mujibu wa Championi Jumamosi, Kapombe alisema amefanyiwa vipimo na wamebaini kwa sasa yupo vizuri na ameanza mazoezi mepesi.

“Nilienda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo ili kujua maendeleo yangu yako vipi, kwa sasa vipimo vinaonyesha nipo vizuri na nimerejea nchini na sasa kuwa mazuri nitaungana na timu kuanza mazoezi lakini kwa sasa namshukuru Mungu niko fi ti kiafya,” alisema Kapombe.

4 COMMENTS:

  1. Rudi mashine rudi wana simba na watanzania wanakumisi.

    ReplyDelete
  2. Wanasimba wana kiu nawe na timu ikijihisi yatima bila nawe unangojewa kwa hamu urejee kilingoni nawe salama salimini

    ReplyDelete
  3. Hongera Simba kwa kujali wachezaji .Kapombe kila mtu anajua moto wako.

    ReplyDelete
  4. Karibu kamanda mpambanaji uwawahi mazembe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic