March 4, 2019






NA SALEH ALLY
MECHI kati ya Yanga dhidi ya Alliance iliyochezwa juzi Jumamosi, imekuwa na malalamiko mengi na makubwa. Lawama inatokea katika kila upande.

Yanga wana imani kwamba walicheza vizuri na kuibuka na ushindi, lakini Alliance wamekuwa wakilalama kuhusiana na bao walilofungwa huku wakisisitiza kwamba haikuwa sahihi maana hata wao walifunga na bao likakataliwa.

Yanga wameibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Bara, hii inawafanya waendelee kuwa mbele wakipambana kuhakikisha wanakuwa mabingwa.

Kwao Yanga ni jambo zuri sana kwa kuwa lengo kuu ni kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wao Simba ambao wana rundo la viporo.

Msingi wa lawama katika mechi hiyo ni jambo la kuangalia kwa macho mawili. Nasema hivyo kwa kuwa tunaweza kujifunza mengi na kutakuwa na usahihi jambo hili likiangaliwa bila ya ushabiki.

Kwamba mwamuzi alikuwa ni mtoa haki sahihi? Nina bahati mbaya moja kwamba mechi hii niliiangalia kwa vipande mtandaoni kwa kuwa sipo nyumbani Tanzania.

Pamoja na hivyo, nimegundua mambo mengi sana ambayo nimejifunza lakini ningependa kuachana na lawama za kazi ya mwamuzi ilivyokuwa na badala yake nijikite katika suala la nidhamu.

Nisisitize, kama mwamuzi hakuwa sahihi basi tuangalie kwa jicho lisilo na ushabiki na baada ya hapo hatua zichukuliwe.

Wakati hatua zinachukuliwa, lazima tuwe tumejiridhisha kuwa kweli kosa lilifanyika na si kuangalia kwa matakwa ya kishabiki maana utani wa Simba na Yanga umegeuka kuwa kama vita, jambo ambalo si sahihi.

Nimeona matukio kadhaa ya wachezaji wa Alliance, hakika si sahihi. Mfano mchezaji mmoja aliyempapasa mchezaji wa Yanga makalio lakini yule aliyemkita mchezaji wa Yanga teke la tumboni na mengine ya namna hiyo ya utovu wa nidhamu unaoonyesha malezi mabovu.
Mimi nimecheza mpira wa uswahilini ambao mchezaji anaweza kuchagua aina yake ya kuwa kwa maana ya kufanya anavyotaka yeye kwa kuwa hakuna malezi ya kisoka.

Vipi leo timu kama Alliance ambayo navutiwa nayo kwa aina ya kiuchezaji kwa kuwa inaonekana soka lao ni la mafunzo.

Nashangazwa zaidi na kuona wao Alliance wanafanya utovu wa nidhamu ambao kamwe hauwezi kufanywa na timu ambayo ina maendeleo ya mafunzo kiuchezaji.

Alliance wamekuzwa katika misingi ya kisoka, hata kama watakuwa na wachezaji wengine wageni ambao wameingia wakijiunga na timu yao bado hawawezi kubadili tabia ya ubora wa kikosi kizima.

Vipi mchezaji kutoka Alliance anaingia katika makundi ya upapasaji makalio ya wachezaji wengine tena katika sehemu ambayo haina purukushani yoyote?

Kwa nini tusione wachezaji wa Alliance wakiwa gumzo la mfano kwa kuwa timu yao imekuwa na malezi sahihi tena ya muda mrefu na wengi wao wamelelewa kama vijana wadogo hadi kufikia hapo walipo.

Huenda Alliance wangeweza kuwa mfano na mwanzo wa mabadiliko la soka ya Tanzania na si kuingia kwenye kundi la kufanya mambo kwa kubabaisha kama ambavyo imeanza kuonekana.

Ushauri wangu kwa uongozi wa Alliance unapaswa kukemea hili kwa wachezaji wake badala ya kukubali liendelee kwa kigezo Yanga ilipendelewa.

Hili halihusiana na Yanga kupendelewa na si jambo jema kwa afya ya soka ya Alliance ambayo ina vijana wengi wanaendelea kukua na hawapaswi kuona upuuzi wa namna hii usiovumilika.

Uongozi wa Alliance lifanyieni kazi hili, limalizeni na kuifanya Alliance iendelee kuwa na afya sahihi ya mapambano muendelezo.

6 COMMENTS:

  1. Unafiki utakuua. Yanga walipofanya madudu katika mechi nä Prisons hukuandika lolote. Wachezaji walimkita mwamuzi tena sio mara moja.Alliance wamefanya makosa ndio lakini wanapofanya makosa wengine uandike vile vile.
    Usichague easy targets .

    ReplyDelete
  2. Hakuna cha unafiki wala nini, Saleh anaongea point ya maana na si vizuri kujaribu kufifisha mauzui yake ya msingi kwenye mada hii. Alliencce school of football? Ile ni timu kutoka shule ya malezi na maadili ya soka Tanzania vipi leo wachezaji wake wanakuwa na tabia za kihuni kuliko hata timu za mitaani?

    ReplyDelete
  3. Mkuu anachosema ni kwamba haki iangaliwe kwa uamuzi sawa. Sio Alliance wahukumiwe kipekee kwa sababu wamefanya kosa nä wengine unaowaita wa mitaani waachwe .
    Hili litavaliwa bango sana kwa sababu Alliance ni timu ndogo.
    Timu zinakataa kuingia vyumbani hakuna hatua yeyote,wachezaji wanapiga marefa hakuna lolote.Timu zinapendelewa waziwazi bila hatua kuchukuliwa kwa muda stahiki.
    Mchezaji anampiga mwenzake mbele ya refa anaachwa acheze mechi anazotaka.
    Justice delayed is justice denied .

    ReplyDelete
  4. Alichokisema mwandishi yawezekana hamjamuelewa, kuna mchezaji wa Alliance alimpiga kidole cha kati matakoni (kidole chuji) Gadiel Michael. Hiyo ndo hofu yake kuwa shule ya soka inaweza ikawa na tabia ile?

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Alichokiandika mwandishi ni sawa kwa spande mmoja na alichokiandika Haji Manara. Wote wamelaani mchezaji wa Alliance kumfanyia kited kile mchezaji wa Yanga. hapo hakuna suala la ushabiki ni kukemea kitendo cha kihuni na kutaka TFF imchukulie hatua kali mchezaji huyo. TFF hawapo kwa bahati mbaya hata ile kamati ya masaa 72 hatujaisikia toka kuahirisha kumsikiliza mchezaji Ninja kupisha kwanza ache zee timu yake. Lipo tatizo kwa chombo kinachosimamia nidhamu za wachezaji uwanjani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic