March 1, 2019


KOCHA wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anatambua mchezo wa kesho dhidi ya Alliance FC ni mgumu ila hesabu kubwa ni pointi tatu mapema kwenye Uwanja wa Kirumba.

Yanga wanaongoza ligi kwa sasa wakiwa wamecheza michezo 25 wamefikisha pointi 61 wakiwaacha wapinzani wao Simba wakipambana kujitoa nafasi ya tatu kutokana na viporo walivyonavyo kwani wamecheza michezo 19 wakiwa na pointi 48.

Zahera amesema amewaambia wachezaji wake kwamba wanapaswa watambue thamani ya kuwa ndani ya Yanga na kazi yao inapaswa iwe tofauti na timu nyingine.

"Nimeona namna tulivyopata taabu kupata matokeo kwa timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ile ya Namungo licha ya ubora waliokuwa nao wapinzani wachezaji wangu walianza kucheza bila kushirikiana mwanzo.

"Makosa yao nimeyarekebisha na nimewaambia mchezo wao wa kesho sio mwepesi wanakazi kubwa ya kufanya, imani yangu ni kuona tunapata matokeo chanya na kubeba pointi tatu kibindoni," amesema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic