March 1, 2019


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Azam FC, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ameshindwa kuondoka nchini Tanzania kwa wakati mara baada ya kutimuliwa klabuni hapo kutokana na kusubiria malipo yake ambayo hajapatiwa.

Azam FC iliachana na Pluijm hivi karibuni kufuatia matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi zao tano ikiwemo kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando, alisema Pluijm ataondoka mara tu baada ya kupatiwa haki yake ambayo bado hajaipata.

“Kocha Hans bado yupo hapa nchini na hajaondoka ila anasubiri akishalipwa ndiyo aweze kuondoka, uongozi unafanyia kazi suala lake na wakati wowote kuanzia sasa mchakato utakamilika.

“Siwezi sema ni kiasi gani anatakiwa kulipwa lakini kila kocha atalipwa kulingana na mkataba wake kwa upande wake yeye Hans na msaidizi wake Juma Mwambusi,” alisema Alando.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic