March 10, 2019


FT Yanga 2-1 KMC
Uwanja wa Taifa


Dakika ya 87 Abdalah Shaibu anaonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 81 KMC anatoka Abdalah Hilary anaingia Sangija
Said Makaku anaingia anatoka Ngassa dakika ya 81. Yanga wamepiga mashuti 3 yaliyolenga lango -6 KMC Karos Kirenge anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 69.

Dakika ya 67 Ally Ally anajifunga bao kwa kichwa akimalizia pasi ya Ajibu. Dakika ya 62 Kaseke anatoka anaingia Ajibu, Kamusoko anatoka anaingia Tambwe.
Yanga wamecheza faulo 7-10 KMC Dakika ya 59 Charlse Ilanfya wa KMC anatoka anaingia James Msuva.

Dakika ya 53 Charlse Ilanfya anapewa huduma ya kwanza baada ya msuli kushtuka, Yanga wanakaza kucheza fairplay.

Kelvin Yondani dakika ya 49 anapewa huduma ya kwanza.

Hasan Kabunda anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 52 baada ya kumchezea rafu Mrisho Ngasa.

Kipindi cha pili, Juma Kaseja anaingia kuchukua nafasi ya Jonathan Nahimana.

Dakika 45 za kwanza zinakamilika inaongezwa dakika moja Makambo anaotea dakika ya 42 ya mchezo kwa sasa.

Mfungaji bao la KMC, Mohamed Rashidi dakika ya 16.
Kwa upande wa Yanga, Papy Tshishimbi anafunga bao dakika ya 38.

Dakika ya 38 Tshishimbi Goooooooo anasawazisha bao kwa kichwa baada ya kona fupi kupigwa kuanzia kwa Kaseke alimpasia Gadiel kisha akatupia pasi iliyomkuta Tshishimbi.

  Dakika ya 35 mchezaji wa Yanga Paul Godfrey anamchezea rafu Kabunda wa KMC ambaye anapewa huduma ya kwanza na kurejea Uwanjani.

Dakika ya 28 Thaban Kamusoko  anaonyeshwa kadi ya njano.

Nahimana mlinda mlango wa KMC anapewa huduma ya kwanza baada ya kulifuata shuti lililogonga mwamba.


KMC kwa sasa wamepaki basi baada ya kufunga bao la kwanza, dakika ya 23 Kamusoko anapiga faulo inayogonga mwamba.


Dakika ya 16 Mohamed Rashid anafunga Gooooooo la kuogoza kwa KMC akiwa ndani ya 18.

Faulo: Yanga 3-3 KMC
Kona: Yanga 1-1 KMC

Kelvin Yondani anapiga shuti kali dakika ya 13 linalopanguliwa na Nahimana na kufanya Yanga wapige kona ya kwanza ambayo haijazaa matunda.

Mpaka sasa dakika 12 zimekatika huku Yanga wakicheza faulo 3 sawa na KMC.

Mchezo unaoendelea kwa sasa ni kati ya Yanga na KMC, Uwanja wa Taifa ambapo kwa sasa ni kipindi cha kwanza.

Mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange huu sio wengi kwa sasa.

Kipindi cha kwanza ushindani huku kila timu ikishambulia kwa zamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic