March 14, 2019


Klabu ya Liverpool imetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuicharaza Bayern Munich jumla ya mabao 3-1 ikiwa Uwanja wake wa nyumbani.

Mabao ya mchezo huo yamewekwa kimiani na Sadio Mane aliyefunga mawili pamoja na beki Virgil van Dijk kwa upande wa Liverpool huku Bayern wakicheka na nyavu mara moja kupitia kwa Joel Matip wa Liverpool aliyejifunga.

Mbali na Liverpool kutinha hatua hiyo, Barcelona pia waliokuwa wakiikaribisha Lyon ya Ufaransa nao wameichapa mabao 5-1 kwenye Dimba la Camp Nou.

Mabao mawili ya Messi moja akifunga kwa tuta pamoja na Phillipe Coutinho akifunga moja, huku Ousmane Dembele naye akitupia pamoja na Gerrard Pique.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic