MALI ZA MANJI ZAZUILIWA KUTOKANA NA DENI
Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini na Mwanachama wa Yanga, Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC
Manji anadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 25 ambazo ameshindwa kuzirejesha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba hivyo kusababisha mali zake zilizopo Mwanza na Dar es Salaam ambazo ziliwekwa dhamana, kuzuiwa
Mali hizo zimezuiwa kwa oda mbili tofauti za Mahakama hiyo, zinazomzuia Manji kufanya muamala wa aina yoyote kuzihusu ikiwamo kuhamisha umiliki kama zawadi, kuuza au kuweka dhamana
NBC ilifingua kesi mwaka 2016 ikizishtaki kampuni za Farm Equip (T) Limited, Tanperch Limited na Quality Group Limited zinazomilikiwa na Kaniz Manji na Yusuf Manji kwa kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15.9 bilioni.
kila linapokuja suala la kufamyika uchaguzi Yanga yanaibuka matatizo mapya ya Manji
ReplyDeletenadhani hili linabidi lichunguzwe kwa undani Zaidi
Kwani wewe binafsi unashindwa nini kuchungunza kwa undani zaidi? uchaguzi na madeni anayodaiwa Manji inawahusu vipi Yanga?
DeleteJuu ya yote haya yanga bado wamo kumuandama kwakutaka hela
ReplyDeleteYaani wasidai madeni yao kwa sababu Yanga wanataka kufanya uchaguzi!!!
ReplyDeleteFikra mufilisi dawa ya deni kulipa sio kutafuta mchawi.
Ujinga ni maradhi.