March 18, 2019


Mafanikio ya Simba kwenye Ligi ya Mabingwa, yameinyanyua Tanzania hadi nafasi ya 12, ambayo ndiyo ya mwisho katika orodha ya nchi zinazopewa nafasi 4 katika mashindano ya Afrika...ahsante Mungu!

Kabla ya msimu huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya 26 na pointi zake 3 zilizotokana na Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, 2016 na 2018. 
Kufuzu kwa Simba robo fainali msimu huu, kumeipatia nchi yetu pointi 15 ambazo zikichanganywa na zile 3 za Yanga, tunakuwa na pointi 18!

POINTI

CAF hupima viwango vya nchi kupitia mafanikio ya vilabu vyake, kwenye mashindano ya Afrika, kwa kipindi cha miaka mitano. Viwango vipya vitakavyotoka vikijumuisha mafanikio ya Simba 2018/19, vitaanzia 2015.

Mwaka wa karibuni zaidi huwa na thamani kubwa zaidi (maksi 5) kuliko mwaka wa nyuma zaidi (maksi 1). Thamani ya mwaka wa mashindano huzidishwa na pointi ambazo klabu huzipata kutokana na mafanikio yake kwenye mashindano husika, na kuwa pointi za nchi.

KOMBE LA SHIRIKISHO

Klabu itakayoshika nafasi ya 4 kwenye makundi, hupewa pointi 0.5. Nafasi ya 3, pointi 1, robo fainali, pointi 2...bingwa pointi 5.

Yanga ilifuzu hatua ya makundi mwaka 2016 na 2018, na kumaliza ya 4 mara zote mbili. 
Thamani ya mwaka 2016 ni maksi 2, maana yake ni 0.5 × 2 = 1. Thamani ya mwaka 2018 ni maksi 4, maana yake ni 0.5 × 4 = 2. 
Kwa hiyo Tanzania ilivuna pointi 3 kutokana na mafanikio ya Yanga, 2016 na 2018!

LIGI YA MABINGWA

Kufuzu makundi tu ni pointi 0.5 na kufika robo fainali ni pointi 3. Simba imefika robo fainali 2018/19 ambao thamani yake ni maksi 5. Maana yake ni 3×5=15.

Pointi hizi 15 zikijumlishwa na zile 3 za Yanga, Tanzania inakuwa na pointi 18. TUMETUSUA!

Hata hivyo, pointi hizi zitaingia kwenye mahesabu kuanzia msimu ujao kwa ajili ya matumizi ya msimu wa mbele yake, yaani 2020/2021.

Hakuna uwezekano wa pointi zetu kuvukwa na nchi nyingine kwa sababu walio chini yetu hawana timu zilizopo kwenye mashindano.

Pia ukiangalia hapo kwenye mchoro, utaona pointi zetu zimewekewa alama ya ≥...hii ina maana kwamba zinaweza kuongezeka, endapo Simba watasonga mbele zaidi.

Imeandaliwa na Zaka Zakazi

6 COMMENTS:

  1. kwa maana kwenye club champions Tanzania itatoa timu 2 au 3?

    ReplyDelete
  2. Ukimiona kanga ndani ya mtego husemi asante kanga lakini asante mtego nasi twasema asante MO kwakuweza kuifikisha Simba hapa ilipofika kwa muda mdogo kabisa ambapo walioshika hatamu kwa miaka mingi hawakufika popote. Mungi ibariki Simba na umbariki alieifikisha simba ilipo hivi sasa.

    ReplyDelete
  3. Asante Yanga kwa point tatu....pamoja na miaka yote ya ubingwa wa historia

    ReplyDelete
  4. Ndipo pale tunaposema zalendo kwanza kwa mechi za kimataifa. Uzalendo ni kuweka maslahi ya Taifa kwanza na hahihisi nani analiwakilisha taifa iwe Yanga, Azam,mtibwa au Simba. Linapokuja suala la mechi za kimataifa ni vyema tukaungana.

    ReplyDelete
  5. Tino we ni noma sana, miaka mingi wameshiriki ila matunda ni kiduchu sana wameipatia nchi aisee labda walikuwa mabingwa by name tu! Wazee wa porini mwaka mmoja tu point 15 duh mnyama anatisha kweli!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic