MASOUD DJUMA AONGEZA TENA NGUVU SIMBA
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Masoud Djuma, amesema anaamini kuwa timu hiyoitapata matokeo katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya AS Vita.
Djuma anaamini kila timu inatumia faida ya Uwanja wake wa nyumbani hivyo anawapa nafasi nzuri Simba ya kupata matokeo wakiwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza kupitia kituo cha EFM Radio, Djuma ameonesha jeuri hiyo kutokana na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika tangu zianze haswa timu zilizo kundi D hakuna hata moja iliyopoteza nyumbani.
Simba itaenda kucheza na Vita Jumamosi hii ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja nyumbani na ikiwa nafasi ya 4 kunako kundi D ikiwa na alama zake 6.
0 COMMENTS:
Post a Comment