March 17, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa hesabu zake ni kuona anapata matokeo chanya kwenye mechi zake zote zilizobaki ili kubeba ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kombe la Shirikisho kutokana na aina ya wachezaji alionao.

Zahera amesema kuwa licha ya ugumu ambao wanapitia kwa sasa anaamini wachezaji wake ndio watafanikisha suala la kubeba mataji kwenye mashindano ambayo wanashiriki hivyo ni suala la muda tu kupata matokeo.

"Ajibu (Ibrahim) akiwa kwenye ubora wake na Makambo (Heritier) akiwa kwenye ubora basi hawa wakiwa ndani ya uwanja sina mashaka na suala la kupata matokeo najua ni suala la muda tu.

"Tambwe (Amiss) yeye anafanya vizuri akitokea benchi kwa kuwa amepindua matokeo mara nyingi na ninamuamini, wachezaji wote wanacheza wakiwa ni timu pia wengine wapo timu ya taifa kama Kelvin Yondani, Feisal Salum, Andrew Vincent na Gadiel Michael, naona tukifanya vizuri licha ya kupitia kipindi kigumu.

"Kwa kila mchezaji ndani ya Yanga anatambua thamani ya jezi ya Yanga na anaheshimu timu yake hivyo malengo yetu yatatimia,"  amesema Zahera.

 Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 28 ikiwa na pointi 67.

8 COMMENTS:

  1. Vipi ubingwa nawe umwakimbia wachezaji wako na huku umeshafungwa mara kadhaa na kwani hujaiona spidi ya mnyama?

    ReplyDelete
  2. Kwa Simba ile ya pale Taifa Yanga ubingwa asahau kwa sasa. Watakachokukifanya Yanga kwenye ligi ni kumuamsha mnyama asijishau Fisi wakaanza kudhania kuwa ni mgonjwa nakuanza kumtia presha.

    ReplyDelete
  3. Kwani bado hajaondoka. Si alikuwa awe Congo leo.Au mission imefeli amekuja na gia ya kuwapooza migongo wazi.

    ReplyDelete
  4. Wallahi ubingwa wausahau ila kama Mungu atafanya miujiza yake

    ReplyDelete
  5. Ni jambo la kustaajabisha sana maneno kama hayo yanga wamekuwa wakiyatumia kila wanapokula vichapo na kupoteza pointi. Yanga wanayo wanayo hisia kuwa wao sio wakufungwa kabisa na wakifungwa wana hisia ni kitu cha aibu jambo ambalo mnyama hanalo. Simba inasema, "-there is no joy in victory without running the risk of defeat"

    ReplyDelete
  6. sasa povu linawatoka la nini hua naona mashabiki wa simba tu wanaweka comment dhidi ya kocha wa yanga na hawajitambui kua yule kocha anawahusu yanga na si simba !!
    fanyeni yenu waacheni yanga na shida zao au na umaskini wao ! mnajivunia utajiri wa kununuliwa ! si bora kutembeza bakuli kuliko kuhongwa maana anaehongwa anajulika ni nani !!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Basi luga kama hiyo chafu ndiyo inayozidisha kuzamisha jahazi kenu lakini tena sikio la kufa halisikii dawa na mutaendelea nayo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic