March 11, 2019


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kimeshtuka baada ya kutoka kipindi kigumu cha kukosa matokeo hali iliyomfanya akae na wachezaji wake kuwapa mbinu mpya zinazowasaida kupata matokeo chanya.

Mpaka sasa Mtibwa imeshinda mechi tatu mfululizo Uwanja wa Manungu baada ya kuanza mbele ya Coastal Union 1-3, Mbao FC 0-2, Stand United 0-2 zote Uwanja wa Manungu.

Katwila amesema kuwa kwa sasa haoni kikosi kitakachompa shida Uwanja wa nyumbani Manungu kazi yake itakuwa ni kuchinja na kubeba pointi tatu.

"Tumetoka kwenye kipindi kigumu na cha mpito kukosa matokeo chanya kwenye ligi, sasa tayari muda wa mpito umekwisha tunaanza kazi rasmi kupata matokeo.

"Anayefuata hapa kesho ni Singida United, tumejipanga kupambana na kubeba pointi tatu hapa nyumbani, mwanzo tatizo la ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa inanisumbua ila kwa sasa hakuna tatizo hilo," alisema Katwila.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic