KOCHA wa timu ya Lipuli FC, ambaye alikuwa nahodha wa Simba zamani, Seleman Matola amesema kuwa Simba wana nafasi ya kuwatungua AS Vita na kutinga hatua ya robo fainali endepo hesabu zao zitakuwa ni kupata ushindi wa mapema.
Simba leo watashuka Uwanja wa Taifa kumenyana na AS Vita ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi ambapo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kutinga hatua hiyo kubwa Afrika.
Matola amesema kuwa anaiona Simba ikipata nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kutokana na mfumo wa kundi ulivyo kwa kila timu kushinda mechi nyumbani pamoja na upana wa kikosi cha Simba.
"Nimelitazama kundi ambalo Simba wapo ni kundi lenye maajabu sana, timu zote hakuna hata moja iliyopoteza nyumbani hivyo hiyo ni fursa kwa Simba kutumia vema Uwanja wa nyumbani pamoja na mashabiki wao.
"Umakini kwa kila mchezaji kuona thamani ya jezi aliyovaa pamoja na nidhamu nje na ndani ya Uwanja vitawabeba Simba na watafanikiwa kushinda mchezo huo ambao ni muhimu kwao, nina amini wakitulia watapenya na kuandika rekodi mpya," amesema Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment