March 18, 2019


Baada ya kuchapwa bao 1-0 juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa, Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, ameeleza kusikitishwa na matokeo hayo.

Akilimali ambaye ni kiongozi mkongwe ndani ya Yanga, amesema hajafurahia kabisa na yamemuumiza kiasi ambacho kimesababisha asiongee mengi.

"Kwakweli matokeo yameniuma mno.

"Siwezi kueleza mengi bali nastahili kupumzika kwanza.

Yanga ilipoteza kwa bao hilo moja likifungwa na Haruna Shamte mnamo dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya faulo.

Kupoteza kwa Yanga kunawafanya wapoteze mechi ya tatu sasa kwenye ligi.

5 COMMENTS:

  1. Yanga wamepoteza kwasababu walijikita wote pamoja na kocha wao Zahera kwenda kuishanglia Vita waishinde Simba badala ya kwenda kuishangilia timu yao kuifunga Lipuli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huo ndio ukweli na ndio sababu kubwa kwa Yanga kula kichapo

      Delete
  2. Nyumba yako inashuka moto unakimbilia kwa jirani kuzima moto. Matokeo ndio hayo. Hasidi hana sababu huvuna anachopanda.
    Ujinga ni maradhi .Pukachaka.

    ReplyDelete
  3. Badala ya kuipa sapoti Simba ambayo kuingia kwake robo fainali kumesaidia kuongezeka kwa timu zetu ktk Africa club champion lkn wenzetu hawalioni hilo na wamebaki kuendekeza ulimbukeni.Zahera alishalisema hilo kuwa kufanikiwa kwa Simba kuingia robo fainali ina maana kuongezeka kwa timu zaidi ya moja toka Tanzania na maana ndio maana alikuwa anapigania timuya kwao ili iingie robo fainali kwa maana Congo msimu ujao Congo iingize timu zaidi ya 4 na ndipo hapo ungesikia Zahera amesepa kurudi kufundisha timu za kwao DRC Congo lkn kwa sasa sidhani ataikacha Yanga sababu ana uhakika Yanga itamaliza nafasi mbili za juu hivyo Yanga itapata nafasi ya kuingia kwenye club champions au shirikisho.Wakati umefika wa kujitadhimini.

    ReplyDelete
  4. Maoni ya kulaumu upande Fulani na kupongeza upande Fulani bado havitatuweka pamoja.Kama nchi kipo cha kujivunia na kujifunza. Tumewapa wageni faida kwa muda sasa. Tunahitaji kuanza upya na kujenga Kuta zetu vizuri. Vita ya familia iendelee lakini inapokuwa ya ukoo familia inabidi kuwa Pamoja.
    Asante.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic