MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Alexis Sanchez amekubali kuondoka ndani ya klabu yake hiyo kutokana na kukosa nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.
Sanchezi ameripotiwa akisema kuwa ataondoka kwenye timu hiyo baada ya kupona majeraha yake ya mguu anayosumbuliwa kwa sasa na anatambua hakuna ni timu chache ambazo zimekuwa zikimuhitaji kwa sasa.
Ole Gunnar Solskjaer Meneja wa Manachester United yupo tayari kumruhusu Sanchezi kuondoka baada ya kuona hawezi kuingia kwenye mpango wake moja kwa moja.
Tangu ajiunge Man United msimu uliopita kwenye dirisha dogo akitokea Arsenal ametupia mabao 3 pekee na kucheza michezo 29 pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment