UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kocha mkuu wa Singida United, raia wa Serbia, Dragan Popadic ni mkorofi akiwa kwenye benchi la ufundi hali inayofanya washindwe kuelewana na kocha msaidizi, Fred Minziro.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa kinachowasumbua kwa sasa ndani ya Singida ni ukorofi wa Popadic unawafanya washindwe kufanya kazi kwa kushirikiana.
"Unajua yule ni mzungu na ana mambo yeke anayoyajua sasa kidogo huwa kunakuwa na kupishana kauli ndani ya benchi, ila haina maana kwamba hawaelewani hapana wanashirikiana vizuri.
"Uongozi uliliona hilo na uliamua kuzungumza nao ili kuweka kila kitu sawa kwa kuwa kwa sasa mwenendo wa timu bado hauridhishi hivyo tuna kazi ya kurejea kwenye ubora wetu," amesema Katemana.
Popadic alitibuana na Minziro kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao walipoteza kwa kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Manungu na jana wakati timu yake inapewa kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Azam alikuwa kwenye jukwaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment