March 4, 2019


BAADA ya jana Simba kubeba pointi tatu mkoani Shinyanga mbele ya Stand United sasa hesabu zao zinabadilika ghafla na kuwa za kimataifa kwa kuwa ndio kituo kinachofuata.

Simba wanatarajiwa kukwea pipa kesho kuifuata JS Saoura nchini Algeria kwa ajili ya kucheza mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa Machi 9.

Beki Kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema ushindani ni mkubwa na kuna tofauti ya ushindani kwenye hatua ya kimataifa hali ambayo inawafanya wajipange vizuri.

"Tumekamilisha kazi ya kwanza kwa muda, sasa kituo kinachofuata ni Algeria, sio kazi nyepesi ambayo tunakwenda kuifanya ila bado tuna nafasi ya kupata matokeo kimataifa.

"Wachezaji wangu wana juhudi na wanafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya mwalimu tutafanya kila njia kupata matokeo ili turejee na ushindi," amesema Wawa.

Simba watashuka kumenyana na Algeria wakiwa na kumbuku ya kushinda mabao 3-0 kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kwenye kundi D ambalo Simba wapo nafasi ya kwanza ipo kwa Al Ahly wenye pointi saba, Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi zao sita, nafasi ya tatu inashikiliwa na JS Saoura yenye pointi tano nafasi ya nne ipo kwa AS Vita wenye pointi nne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic