March 13, 2019


NAIBU Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, ambaye ni mwanachama wa Yanga, juzi aliunga mkono kampeni ya kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera kwa kuanzisha rasmi kampeni ya kutembeza bakuli kwa wanachama wa timu hiyo waishio mikoa ya kanda ya kati kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni moja.

Mavunde ambaye amechaguliwa na Yanga kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji, juzi alianzisha rasmi kampeni hiyo ya kuzungusha bakuli.

Akizungumza wakati wa kampeni hiyo, Mavunde alisema kuwa pamoja na kuhakikisha anatekeleza sawasawa jukumu hilo, pia ameutaka uongozi wa Yanga kuwatambua wanachama wote wa mikoani kwa kupitia kadi zao za uanachama ili waweze kuhakikisha wanalipa michango yao ya kila mwezi ili kuinua njia ya mapato sahihi.

“Nimeamua kuanza kutekeleza wajibu wangu kama mwenyekiti wa hamasa lengo ni kuona tunapata fedha nyingi zitakazoisaidia timu yetu kujinusuru katika wakati huu mgumu tunaopitia pamoja na kwamba nimeanza kwa kukusanya zaidi ya milioni moja kutoka kwa wadau wetu.

“Mbali na hivyo pia tupo katika mbio za kugombea ubingwa na tayari tupo nafasi ya kwanza tukiongoza ligi, hivyo nia yetu tunajitahidi kufanya hivi ili tuweze kuwapa nguvu wachezaji wetu na kocha wetu ambaye anajitoa sana kwa ajili yetu ili aweze kutwaa kombe,” alisema Mavunde.

4 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Huyu ni Waziri wa Serikali. Zipo Sheria za nchi zinazosimamia shughuli za ukusanyaji wa fedha kutoka kwa Wananchi. Ni vema zikaangaliwa na kuzingatiwa zisije muingiza Waziri wetu kijana kwenye Kashfa na uvunjaji wa Sheria.

    ReplyDelete
  3. Acheni uchonganishi yeye ni mwanachama na mpenzi ana haki ya kiraia na utashi binafsi kupenda klabu yeyote

    ReplyDelete
  4. Yanga kuweni makini na maamuzi yenu ya kuhairishahairisha uchaguzi na kutoa mianya ya kuleta sintofahamu fanyeni hiyo mikutano yenu haraka na muwasihi wanachama kuacha kukimbilia mahakamani kufungua kesi na kuleta mshikamano na umoja haraka sasa uchaguzi ufanyike mwezi 4 mkutano mkuu wa wanachama ufanyike mwisho wa mwezi 3. Ili mchakato uende haraka na muwe na uongozi unaosimamia timu kwa ufanisi....muende kwenye mfumo wa uwekezaji kuanzia mwezi 6. Fanyeni haya haraka mko nyuma sana!!!!!...leteni wawekezaji kuunda kampuni ya michezo ya Yanga kuanzia juni Mwekezaji aanze kutafutwa kuanzia mwezi 5....huo ni ushauri wangu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic