YANGA WAIPA MCHONGO STAND UNITED KUIMALIZA SIMBA
KIKOSI cha Simba, Jumapili hii kinashuka uwanjani kupambana na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Simba itashuka katika mchezo huo, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa nguvu hivi karibuni ilipopambana na Lipuli FC huko mkoani Iringa ambako ilishinda mabao 3-1.
Hata hivyo, uongozi wa benchi la ufundi la Stand United, umeweka wazi mipango yake iliyojiwekea kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo mbinu hizo zinahusiana na timu ya Yanga ambayo ni mahasimu wakubwa wa Simba.
Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo na mbinu watakazotumia kupata ushindi katika mechi hiyo hazitakuwa na tofauti sana na zile walizozitumia dhidi ya Yanga na wakafanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0.
“Tunaiheshimu sana Simba, lakini katika mechi yetu ya Jumapili tutahakikisha tunaibuka na ushindi kutokana na mikakati yetu tuliyojiwekea.
“Mbinu ambazo tulizitumia tulipocheza na Yanga, ndiyo hizo tutakazotumia dhidi ya Simba ambayo ina washambuliaji wengi wazuri ambao tayari tumeshapata mbinu za kutosha kuwazuia kuhakikisha hawaipenyi ngome yetu,” alisema Bilali.
Simba kwa sasa ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi, 48 wakati Stand United yenyewe ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 33. Yanga ndiyo inayoongoza msimamo huo ikiwa na pointi 61.
We sema tu mwisho wa siku utalia sana
ReplyDeleteKabla ya kuropoka ilibidi kujifunza kwa walokuwa na kele nyingi na baada ya kichapo kuangukakia pua na kutoweka
ReplyDeleteYanga kabla ta kuwapa mchongo wenhine, kwanza ijipe mchongo wenyewe au kujipatia point 62 ndio wanaona mambo yamekwisha HAHAAA
ReplyDeleteStand ndo wa kumfunda yanga, sio yanga kumfunda stand kwa sababu mfundaji alidundwa na mfundwa.
ReplyDeleteYaan wanapata mbinu kwa m2 tlie mfnga sisi
ReplyDeleteNever fear an army of lions led by a sheep. but fear an army of sheep led by a Lion
ReplyDeleteSasa wenyewe walipigwa moja bila,wakapigiwa mpira mwingi sana ,watasaidianaje na walio wapiga
ReplyDelete