MRISHO MPOTO AMWITA DIAMOND AMZIKE RUGE
MSANII wa muziki wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto, maarufu kama ‘Mjomba’ amevunja ukimya na kumtumia ujumbe wa wazi msanii mwenzake, Diamond Platnumz, kwa kumjulisha kuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefariki dunia hivyo ahudhurie katika msiba huo.
Mrisho Mpoto kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kwa majonzi akisema; “@diamondplatnumz Nasib Abdul nimekwita jina lako la kuzaliwa mimi kama kaka yako unaeniheshimu na kunisikiliza nakwambia. RUGE MUTAHABA AMEFARIKI nakuomba NJOO UMZIKE… Nimemaliza.
Aidha, kauli hiyo ya Mrisho Mpoto imepingwa vikali na baadhi ya mashabiki wake katika mtandao huo wakidai kuwa hakuna haja ya kumbembeleza Diamond kwenda msibani, kwani hata asipokwenda bado Ruge atazikwa na wapendwa wake.
Diamond ambaye alishawahi kupitia kwenye mikono ya Ruge Mutahaba kipindi cha nyuma kabla ya kuwa maarufu, amekuwa kimya mpaka sasa, si kuposti mitadaoni au kufika msibani jambo ambalo limeibua minong’ono miongoni mwa wadau wa muziki nchini na wananchi wa kawaida.
Hivi karibuni, ilidaiwa kuwa Diamond na Lebo yake ya WCB wameingia kwenye bifu kali na Ruge Mutahaba kwa madai ya kutokubaliana kimaslahi kuhusu mambo ya sanaa ya muziki.
Hata hivyo, watu wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu nini atakachokiandika au kukisema Diamond kuhusu msiba huo kwani tangu Ruge aanze kuugua hakuwahi kuonyesha moja kwa moja kuguswa na tatizo hilo na hata hadi umauti ulipomfika.
0 COMMENTS:
Post a Comment