March 16, 2019


Bao pekee la Haruna Shamte mnamo dakiak ya 19 limeinyima alama tatu muhimu Yanga kwa kuipa ushindi Lipuli FC wa bao 1-0.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa umemalizika kwa matokeo hayo ambayo yamekuwa na machungu kwa wadau na mashabiki wa Yanga.

Yanga imepoteza mechi huku Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera akiwa jijini Dar es Salaam baada ya kusema anataka kusafiri kuelekea Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa.

Matokeo haya yaifanya Yanga kusalia kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na alama zake 67 huku Lipuli wakifikisha alama 44 kwenye nafasi ya nne.

Mechi inayosubiriwa hivi sasa ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba itakuwa inacheza dhidi ya AS Vita ya Congo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

7 COMMENTS:

  1. Mbona mmeandika kinyonga.Timu yenu pendwa imefungwa.

    ReplyDelete
  2. Mbona mmeandika kinyonge.Timu yenu pendwa imefungwa.

    ReplyDelete
  3. DU!Kwa hivyo Zahera kaamua kuitelekeza sababu ya As vita? Yaani Zahera ameamua kuutoa kafara ubingwa wa Yanga zidi ya As vita yake? Tatizo ni kwamba Zahera anaona kuifundisha Yanga kama vile anatoa hisanai yaani kama vile anawasaidia.Na ndio pale tunaposema watanzania tusikubali kirahisi rahisi mtu kukwambia atakusaidia halafu ukaanza kushangilia kama vile Fisi alieona mzoga. Msaada mara nyingi gharama yake ni fedhehea na kubwa kuja kuilipa kuliko kujitegemea mwenyewe.

    ReplyDelete
  4. Sio baada ya kusema anataka kusafiri,ni kwamba anasafiri kwenda Congo kesho kwa majukumu ya kitaifa,na hii si Mara ya kwanza,Mara kadhaa amekua akisafiri na timu inapata matokeo bila,ameijenga na kuisaidia Sana timu ktk kipindi hiki cha choka mbaya yanga lkn bado imekua ikipata matokeo,kilichotokea Leo iringa ndio mpira ulivyo watu wa mpira tunaelewa,inawasumbua watu wa simba na yanga,kwa watu wa mpira kawaida sana

    ReplyDelete
  5. nguvu kubwa ilibaki dar kwa AS Vita

    ReplyDelete
  6. متابعة مباريات ليفربول من مصر
    تركيب دش في التجمع الخامس

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic