March 24, 2019


BAADA ya kuonyesha uwezo mzuri kwenye mechi dhidi Yanga, beki wa Simba, Zana Coulibaly raia wa Burkina Faso ambaye alikuwa akijiita Amber Rutty, sasa amesema asiitwe tena jina hilo.

Zana alijiita jina hilo kufuatia mwanzoni kupata shida na kuchekwa na mashabiki wa mitandaoni kwamba siyo mchezaji mzuri lakini baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Yanga na yeye akionyesha kiwango cha juu aliposti picha na kuweka ujumbe uliosema kwamba wanamuita ‘Zana Ambairut’ Amber Rutty.

Zana alisema kuwa kwa sasa hataki kujiita jina hilo na anatamani atoe tangazo kwa kila mtu ili atambue kuwa hapendi tena kusikia yeyote akimuita jina hilo. 

Alisema jina hilo siyo jina sahihi bali lilitokea tu mwanzo baada ya kuona anaitwa na wachezaji wenzake kambini na mazoezini bila kufahamu maana yake.”

"Nimeshajua maana ya jina hilo na nimeonyeshwa mtu mwenye jina na sababu iliyolifanya jina hilo kuwa maarufu nchini, hivyo sifurahishwi tena na matendo ya mwenye jina hilo na nisingependa kumsikia mtu yoyote ananifananisha naye,” alisema Zana.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic