April 26, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee katika klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania kugawa alama moja kwa Simba na KMC baada ya mchezo wa jana.

Akilimali amesema kama TFF wamemfungia Kambuzi na wasaidizi wake waliochezesha mchezo wa jana basi na maamuzi yabadilishwe ili kuweka usawa.

Ameeleza kuwa mechi hiyo ilipaswa kwenda sare ya bao 1-1 lakini kufeli kwa waamuzi kulisababisha KMC wanyimwe penati na badala yake wakapewa Simba baadaye.

Hata hivyo, Akilimali amesema kuwa anajua bingwa wa msimu huu ameshapangwa hivyo wala hapepesi kuumiza kichwa hivi sasa.

"Unajua hawa TFF wanapaswa kuwapa Simba alama moja pamoja na KMC kwa sababu mechi hiyo ilipaswa kumalizika kwa sare ya 1-1.

"Kilichofanyika ni kuibeba tu Simba na TFF wanapaswa kubailisha maamuzi baada ya kuwafungia Kambuzi na wenzake kwa makosa ya uwanjani.

"Najua bingwa ameshapangwa kwa hiyo sioni tatizo na wala siumizi kichwa juu ya nani aatachukua kikombe."

8 COMMENTS:

  1. Nyie Yanga ubingwa wa kazi gani mtakuja kushindwa hata nauli yakwendea Rwanda.TFF ndio wanaovuruga taswira yote ya mchezo wa soka hapa nchini kwani panapostahiki kutoa adhabu hawatoi na pasipostahiki kutoa adhabu ndio wao wanatoa tena kwa haraka. Mchezaji kweli kaushika mpira katika eneo la penalt na kauzuia mpira usiende ulipokusudiwa kwenda sasa unataka mwamuzi afanye nini pengine waamuzi wasingetoa ile penalt wangeingia kunako lawama kubwa zaidi vile vile ila hii TFF we acha tu.

    ReplyDelete
  2. Akilimali huna akili na yanga wenzako,hata wanayanga wenzako hawakupendi mzee unaropoka kama shosti, we mwanaume komaaa acha kelele za kishoga

    ReplyDelete
  3. kubebwa jana kweli simba kabebwa, kama kumrudishia wako kipa mpira inazalisha offside akilimali asingetokwa povu, akishika okwi mpira umefata mkono wakishka wao mkono umefata mpira

    ReplyDelete
  4. Vyura mtapata shida sana na mtateseka mnoo

    ReplyDelete
  5. Vyura nendeni FIFA. Anafungwa KMC lakini wanaumia vyura.Wengine wamekuwa marefa. Wanatafsiri sheria.Aliporudisha mpira Shaibu kwa Kakolanya akafunga Okwi na refa akasema offside mbona hakumutafsiri sheria siku hiyo?
    Ikitokea kwa Simba nongwa ikitokea kwa Chura sawa!

    ReplyDelete
  6. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete
  7. Sijawahi kuona urafiki wa mbuzi na simba, sasa simba kamponza mbuzi wamemwondoa kwenye malisho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic