April 26, 2019


UONGOZI wa Yanga umeamua kuvuja ukimya na kutoa maamuzi mengine kuhusu mgomo wa wachezaji wao kwa kusema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kupata pointi tatu mbele ya Azam FC.

Jana wachezaji wa Yanga waliripotiwa kugoma kufanya mazoezi huku kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera akitoa onyo kwa wale ambao wangegoma kutokea leo kufanya mazoezi kwamba hatawatumia mpaka msimu ujao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa leo wamekaa na wachezaji pamoja na Zahera ili kutatua changamoto za wachezaji na wamepata muafaka wa matatizo yao.

"Jana kulikuwa na kutoelewena kati ya wachezaji na viongozi hali iliyopelekea kushindwa kutimiza majukumu yao, ila leo tumemaliza kila kitu na kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC.

"Kwa sasa kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kupambana na hesabu zetu ni kuona tunapata matokeo chanya, hivyo mashabiki wasiwe na hofu wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu utakaochezwa uwanja wa Uhuru," amesema Saleh.

Azam FC itaikaribisha Yanga kwenye mchezo wa kwanza kwao msimu huu utakaochezwa uwanja wa Uhuru.

3 COMMENTS:

  1. Duh saleh jembe na magazeti ya championi mumeamua kuishambulia Yanga aya bwana endeleeni na chuki na vita zenu dhidi ya Yanga!

    ReplyDelete
  2. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete
  3. Jini limevamia tena yanga kunakuwaga na nn hatua za mwisho duuuuuuuuh!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic