April 26, 2019



KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa kwa hasira walizonazo kwa sasa lazima waanze kumchapa Simba ili waongeze kasi ya kubaki ligi kuu na kuheshimiwa na wapinzani kwenye mchezo wa kesho uwanja wa Karume.

Kocha wa Biashara United, Said ambaye alikuwa kocha wa kwanza kumzidi mbinu mbelgiji wa Simba alipokuwa Mbao kwa kumchapa bao 1-0 amesema kuwa ni lazima washinde mchezo wao dhidi ya Simba kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.

"Hatupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa, naona Simba wanavyokuja kwa kasi na spidi yao naiona ila hiyo hainipi mashaka kwa kuwa naitambua vizuri Simba hawanitishi.

"Tumeitazama Simba namna inavyopambana kuanzia ilivyokuwa hatua za kimataifa pamoja na michezo ya ligi, kasi yao na makali yao nimeshaitambua hivyo nimewapa kazi maalumu wachezaji wangu kuifanya hivyo wakifuata maelekezo poini tatu zinatuhusu," amesema Said.

Biashara United imecheza michezo 31 ikiwa nafasi ya 19 ina pointi 34 kibindoni zinazoiweka kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja msimu ujao.

1 COMMENTS:

  1. Anataka kupatia point kwa Simba yaan huyu kocha mngu Anam muona

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic