April 27, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amezidi kusisitiza kuwataka Wanayanga kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji kura Mei 5 mwaka huu.

Akilimali amesema inabidi wanachama wa klabu hiyo watimize jukumu la haki yao kwa kuhakikisha wanapata nafasi ya kupiga kura kuchagua kiongozi ambaye anafaa.

Ameeleza Yanga ni klabu kubwa na wanaopaswa kupiga kura wanatakiwa kuangalia kiongozi mwenye dira ya maendeleo ndani ya Yanga na si kwa kutazama umaarufu wa mtu.

Aidha, Akilimali amesema ataungana na wanachama wote wa Yanga watakaoenda kupiga kura siku hiyo akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wazee kwani ndoto yake imekuwa ni kuona klabu hiyo inapata uongozi.

"Nawataka wanayanga wote kutimiza haki yao ya kikatiba kwa ajili ya kuhakikisha wanaenda kupiga kura Mei 5.

"Kinachotakiwa hivi sasa ni kulipia kadi zao za unachama ili watimize zoezi hilo.

"Tunapaswa kuchagua kiongozi mwenye sifa nzuri na atakayeisaidia klabu kufika pazuri zaidi." amesema.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic