Barcelona imefanikiwa kutetea taji lao la Ligi ya Hispania La Liga baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Levante lilolofungwa na mshmabuliaji Lionel Messi.
Muargentina huyo ambaye alikuwa akisugua benchi na bao lake aliingia kipindi cha pili na kupachika bao hilo pekee lililoipa ubinwa timu yake.
Barcelona inabeba ubingwa ikiwa ina mechi tatu mkononi za kucheza ili kukamilisha mechi zao za La Liga.
Hili ni taji la nne kwa Barcelona wameshinda ndani ya misimu mitano iliyopita na wana matumaini ya kuchukua mataji matatu msimu huu.
Baada ya kuchukua Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Ulaya wapo nusu fainali na wameingia fainali ya Kombe la Mfalme.








0 COMMENTS:
Post a Comment