April 26, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa haujamjumuisha beki kisiki Pascal Wawa kutokana na kusumbuliwa na majeraha hivyo kesho hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Biashara United.

Simba jana imemaliza biashara mbele ya KMC na kusepa na pointi tatu leo imetia timu mkoani Mara na kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Biashara United.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa tangu mwanzo hawakuwa na mchezaji Wawa ambaye anaendelea kupata matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe.

"Hatujaongozana na Wawa tangu mwanzo wa mechi zetu za kanda ya ziwa kwa kuwa bado hali yake haijawa sawa ila kwa wachezaji ambao tupo nao kambini wote wapo salama na kesho wataivaa Biashara kwa nguvu zote endapo," amesema Ally.

Mchezaji mwingine wa Simba ambaye bado hajarejea uwanjani kwa muda mrefu ni Shomari Kapombe ambaye mashabiki wamemkosa kutokana na kuendelea kutibu majeraha yake ya mguu, ila tayari ameanza mazoezi mepesi na muda wowote ataanza kuonekana uwanjani kwa mujibu wa Dr. Yassin Gembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic