April 26, 2019


MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti ndani ya Yanga, Dk Jonas Tiboroha na wagombea wenzake wa awali, wanasubiria maamuzi ya kamati ya rufaa za uchaguzi ya TFF ili kuwajua wapinzani wao kwa ajili ya kuanza mchakato wa kuwania nafasi mbalim bali za uongozi ndani ya klabu hiyo.

Yanga kwa sasa ipo katika mchakato wa kufanya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo Mei 5, mwaka huu kwa kuziba nafasi zote zilizo wazi ambapo kwa sasa wanasubiria rufaa iwapo wagombea walioenguliwa watafanya hivyo ili kupeleka majina hayo katika Kamati ya Maadili ya TFF kisha kuwaunganisha.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF hivi karibuni iliwaengua baadhi ya wagombea akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga, Hussein Nyika kutokana na kutokidhi vigezo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela amesema kuwa, kwa sasa bado wanasubiria tarehe ya kukata rufaa ifike ili kujua waliokata rufaa na kujua wafanye nini na iwapo ikitokea hakutakuwa na mtu wa kufanya hivyo majina hayo yatapelekwa katika kamati ya maadili kisha watakaopitishwa ndiyo watakaoungana na kina Tiboroha.

“Wagombea wa mwanzo wanatarajia kuungana na wenzao mara baada ya Kamati ya Maadili ya TFF kupitia majina yote ya wagombea na ndipo tutakapowajumuisha wote watakaoingia katika kinyang’anyiro hicho,” alisema Mchungahela.

2 COMMENTS:

  1. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumia akili wewe usiropoke tu kwani Mwinyi anamiliki vyombo vya habari au yeue ndo anawaambia waandishi waandike habari za Yanga? Duuh kweli mbumbumbu ni mbumbumbu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic