CHAMA: TULIENI DAWA ITAWAINGIA
KIUNGO mpaka rangi wa Simba, Clatous Chama raia wa Zambia, amehuzunika kwa kushindwa kuwafunga TP Mazembe kwenye Dimba la Taifa lakini akaweka wazi kwamba hukohuko kwao DR Congo watafungika.
Mzambia huyo juzi Jumamosi alikuwa mmoja wa viungo walioanza katika kikosi cha Simba katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe. Mechi hiyo ilimalizika kwa suluhu.
Timu hizi mbili zitarudiana Aprili 13, katika mechi ya pili itakayopigwa Lubumbashi, DR Congo kuamua timu itakayofuzu nusu fainali.
Kiungo huyo mwenye miaka 27 amesema kuwa matokeo hayo kwao hayakuwa bora sana lakini watapambana katika mechi ya Congo ili wapate ushindi.
“Hatukuwa tunataka mechi hii imalizike kwa matokeo ya namna hii. Lakini kuna nafasi ya pili tutafanya kile kitu ambacho tumeshindwa kukifanya hapa Dar,” alisema Chama mwenye mabao matano katika Ligi ya Mabingwa.
Mazembe wanahofu tayari tamu zaidi jeshi la Mazembe lilokuja Dar lilikuwa jeshi la kikosi cha kwanza cha maangamizi lakini waliponea chupu chupu kuliwa na Mnyama. Kwa Simba kupata bahati ya kuiona picha halisi ya Mazembe kiufundi hapana shaka kazi ipo Lubumbashi na lolote linaweza kutokea na kuwastajabisha wengi ngoja siku ifike kunako uhai ila Simba nafasi wanayo tena kubwa ya kusonga mbele.
ReplyDeleteNna hofu na kifurushi kipya tuu
ReplyDeletekule watapigwa thamaniya 8
ReplyDelete