April 28, 2019


KOCHA Mkuu wa KMC, Ettiene Ndiyaragije amejiwekea rekodi yake ya kipekee kwenye Ligi Kuu Bara kwa kutoa sare nyingi kwenye michezo yake aliyocheza kuliko timu nyingine.
Mpaka sasa KMC imecheza jumla ya mechi 32 ambazo ni sawa na dakika 2,880 huku akishinda mechi 9 ambazo ni sawa na dakika 810 na kupoteza mechi 8 ambazo ni sawa dakika 720.
Rekodi inaonyesha kwamba kwenye ligi kuu hakuna timu ambayo imetoa sare nyingi kama ambavyo imefanya KMC ambapo mpaka sasa ina sare 15 ambazo ni sawa na dakika 1,350.
Timu nyingine ambayo inafuatia kwa kutoa sare nyingi ni Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda ikiwa imecheza mechi 33 sawa na dakika 2,970 huku akitoa sare 14 sawa na dakika 1,260.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic