April 25, 2019


MWENDO kasi ndiyo ligi yetu kwa sasa inakwenda ukizubaa unaachwa kwani hakuna ambaye hana hesabu za kushinda michezo yake kwa sasa iliyobaki ndani ya ligi kuu hasa ukizingatia ni mwendo wa lala salama sasa umeshikiliwa.
Kuna timu ambazo zina subiri michezo yao kwa muda mrefu hii ni sawa na kusema kwao ni kipindi cha mapumziko na huo ni muda wa kurekibisha makosa ambayo waliyafanya wakati uliopita na kushindwa kupata matokeo kwenye michezo yao.
Pia zipo timu ambazo zinamalizia michezo yao iliyobaki hasa baada ya kucheza michezo mingi ambayo imewafanya wajijue wapo eneo gani na mahali gani wanakwenda kwa sasa kutokana na matokeo ambayo wameyapata kwenye michezo yao ambayo wamecheza.
Hata zile ambazo zinamalizia viporo zipo zinaendelea kupambana na hili ndilo linatakiwa kutokana na kwamba mwisho wa siku ni lazima kila mchezaji atimize majukumu yake na timu icheze michezo yake yote.
Mwenendo unakwenda kama ambavyo umepangiliwa licha ya makosa ambayo yanatokea hasa kwenye upangaji wa ratiba ni jambo ambalo linahitaji tiba mapema msimu ujao kila kitu kiwe kwenye mpangilio mzuri.
Bodi ya Ligi Tanzania kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatakiwa liyaone haya ambayo yametokea msimu huu hasa kwa timu kupishana idadi za michezo hili halipo sawa linaua ushindani uliopo kwenye ligi.
Timu ambayo itapata matokeo ni ile ambayo itajipanga vema na kupiga hesabu ambazo zitaifanya ipate matokeo na sio manenomaneo hakuna kitu kama hicho kinaweza kutokea kwenye ulimwengu wa mpira Duniani.
Wengi ambao wamekuwa wakilaumiwa hasa baada ya michezo kuisha ni waamuzi kutokana na kushindwa kumudu mchezo hili ni jambo ambalo linapaswa litiliwe umakini na mkazo mkubwa ili kupunguza lawama na makosa ambayo yanatokea.
Waamuzi wachezeshe michezo yote kwa kufuata sheria 17 za michezo ili kumudu na kusimamia ule utaratibu ambao umewekwa na sio vingenevyo kwani lawama zimekuwa nyingi kwa sasa kwa timu ambazo zinapoteza michezo yao.
Wachezaji pia wasisahau kutimiza majukumu yao ipasavyo wawapo uwanjani kwa kupambana kwa hali na mali kupata matokeo na sio wawe ni mafundi wa kutafuta sababu pale wanaposhindwa.
Kazi ya benchi la ufundi iwe ni kutatua yale matatizo ambayo yanatokea baada ya mechi na kusahihisha makosa ambayo yanatokea hali itakayosaidia kuwa na matokeo chanya kwenye michezo mingine ambayo inafuatia kwa timu na sio kurudia makosa.
Kama kila mmoja atatimiza majukumu yake inakuwa ni rahisi kupata matokeo chanya uwanjani na kuendelea kujiweka sehemu nzuri kwa timu kufikia malengo ambayo yamewekwa mwanzo wa msimu na kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi.
Niwakumbushe kwamba sasa hakuna muda wa kupoteza ngoma inapoisha sasa kila mmoja anapata kile alichokipanda kama ni kushuka daraja ama kusalia ndani ya ligi kwa msimu ujao wa mashindano.
Imekuwa ngumu wengi kuamini kwamba kila kitu chenye mwanzo kina mwisho ila huo ndio ukweli kama wachezaji watajidanganya kwamba kesho wana mchezo utakaowasaidia kubaki ndani ya ligi ama watabeba pointi tatu za kesho hilo halipo tena.
Ushindani uendelee kuwa mkubwa kila siku na inaleta raha kwa kuwa kuna vipaji na watu wenye uwezo wanaonekana kikubwa hata kwa wale ambao wanapigia hesabu kubeba kombe ni lazima wapambambane kupata matokeo chanya uwanjani.
Kwa upande wa mashindano ya Afcon kiukweli hali ni mbaya na tumeabika kiasi kikubwa tukiwa waandaaji wa mashindano makubwa ambayo ni mara ya kwanza kufanyika nyumbani kwenye ardhi ya Tanzania.
Tumepata pigo kubwa ambalo huwezi kulisimulia kwa mwingine akakuelewa vizuri hasa ukizingatia sisi tulikuwa wenyeji na tulitambua tutayaandaa haya mashindano bila kujali ni namna gani tutapambana.
Hili ni jambo ambalo linapaswa liwe funzo kwa TFF pamoja na wachezaji wenyewe kuona namna ambavyo wameshindwa kupata kile ambacho wamekiomba hasa kutokana na ushindani ambao wameonyesha tangu mwanzo walikata tamaa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.
Ikumbukwe kwamba haya yote yanatokea ikiwa sisi wenyewe ndio waandaaji, tupo nyumbani tunapoteza tena kwa vipigo vikubwa ambavyo havina idadi hasa kwenye michezo yote mitatu ambayo tumecheza.
Tulianza kufungwa mbele ya Nigeria mabao 5-4 kabla ya kushtuka tukaongezewa mabao 3-0 na Uganda na tukamaliza kwa kufungwa na Angola mabao 4-2 hii ni mbaya na tumepoteza nafasi kubwa na ya muhimu ambayo ambayo tuikuwa tunaweza kuimudu kwa kuwa ilikuwa mikononi mwetu.
Ilikuwa ni muhimu kupata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa na ya kimataifa kwa kushinda mechi mbili za mwanzo ilikuwa ni tiketi ya kwenda Brazili kushiriki kombe la Dunia hatua kubwa ya maendeleo kwenye soka ila ndio hivyo tumepishana nayo.
Nadhani kama timu tungejiandaa vizuri ingetupa matokeo chanya kwani makosa ambayo walikuwa wakiyafanya vijana ni ya kujirudia hali inayoonyesha kwamba hakukuwa na uhakika wa kile ambacho tunakifanya na ndio maana tumetolewa moja kwa moja bila kushinda hata mchezo mmoja.
Wachezaji wangejitambua awali na kujitoa kwa moyo ingekuwa rahisi kwetu kupata mpenyo na kupenya kwenye hatua ngumu ambayo tuliamua kuichagua wenyewe na matokeo yake tunajuta kupoteza na kubaki kuwa watazamaji kwenye ardhi ya nyumbani.
Hatuna uwezo wa kubadili matokeo ambayo yametokea tunachotakiwa kukifanya ni kuanza kujipanga upya wakati ujao hili halikuwa fungu letu ama kama lilikuwa fungu letu tulibweteka na kuacha kufanya ushindani ambao unastahili kwenye michuano hii mikubwa Afrika.
Tujipange licha ya kupoteza nafasi adimu ambayo tuliipata iwe ni funzo na kuona kwamba bila maandalizi hatuwezi kupata matokeo chanya na hata kama itatokea ukawa nyumbani yule aliyejiaanda anakuchapa na kukuabisha kweupe hivyo maneno maneno tuache.
Kama tungeenda Brazili tungewatoa wengi kimataifa na kutengeneza Taifa lenye wachezaji wenye uwezo ila nafasi ndio hiyo tumeiacha huku sisi tukiwa ni wasindikizaji muda mwingine tujipange kufanya makubwa zaidi ya hapa.

1 COMMENTS:

  1. Mi niongelee tatizo la Afcon, huyo kocha (Oscar Mirambo) aliyepewa hiyo timu hana uzoefu wowote wa kukadhibiwa timu yenye kushiriki mashindano makubwa kama hayo. Tatizo chama cha soka kinafanya kazi kama kwa majungu hivi?

    kitu gani kilichosababisha yule kocha wa kwanza aliyekuwa mzuri na wakaja wakampa timu huyu Oscar??

    Mi naona matokeo haya yawe ya TFF ili waache kukurupuka na maamuzi yao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic