April 25, 2019


Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na Timu ya Taifa ya Misri Juni 13,2019 Bourg Al Arab, Misri kujiandaa na Fainali za Afrika (Afcon2019).

Stars imefuzu kushiriki michuano ya Afcon baada ya kushinda mchezo wa mwisho mbele ya Uganda kwa mabao 3-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwenye makundi ya Afcon imepangwa kundi C ambalo lina timu kama Kenya, Algeria na Senegal ambao ndio wataanza kucheza nao kwenye mchezo wa kwanza nchini Misri. 

1 COMMENTS:

  1. Moja ya tatizo la Taifa stars ya sasa imejaa mizengwe katika uteuaji wa kikosi chake na haijulikani sababu ni nini? Kama ni nidhamu basi nidhamu ya kwanza anayohitajika mchezaji kuwa nayo ni uwezo wake uwanjani.Tumeshuhudia Taifa stars ikiwaacha wachezaji wenye uzoefu na uwezo wa kuunda kikosi imara kwa sababu zisizo za msingi wakati moja ya kazi kubwa ya professional coach ni ule uwezo wake wa kudili na wachezaji wenye tabia tofauti au tata na kuwafanya kuwa msaada kwa timu. Kocha anaetumia nguvu tu katika maamuzi ni yule asie na uzoefu na ubora wa taaluma wa kazi yake. Kama uteuzi wa kikosi cha Taifa stars utafanywa kwa utazingatia uweledi na kuondosha siasa za kijinga basi upo uwezekano wa Tanzania kuwashangaza wengi Afcon. Jambo moja la kusikitisha katika uteuzi wa kikosi cha Taifa stars ni pale wanapoita kikosi hicho bila yakuwa na mchujo wa awali wa maana wakati hata Spain licha yakuwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo wa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza lakini katika kujiridhisha lazima huwa na pre selection au kikosi cha awali . Kuna shida gani kwa Taifa stars kuita wachezaji kama sitini 60 au hata 70 na kuwafanyia mchujo wa vitendo na kupata wachezaji husika? Kwani hata Uganda wanafanya,Misri wanafanya,Congo Drc wanafanya kwanini sisi tusifanye ili kujenga kikosi bora. Uzuri wa kuwataja au kuwaita wachezaji kwa ajili ya timu ya Taifa baada ya kazi ya awali ya majopo wa makocha wa ndani hasa wa ligi kuu ni kumjenga mchezaji husika kisaikolojia hata kama hatapita kwenye kikosi cha kwanza la msingi ni kumfahamisha mchezaji husika kujieka tayari kwa ajili ya kuitumikia timu ya Taifa muda wowote ule kama atakuwa hakupita kwenye mchujo. Hii inamueka mchezaji katika hali ya kujitambua zaidi. Sina uhakika wa ushiriknao kati ya Amunike na makocha wa ligi kuu lakini ili taifa stars kupata wachezaji wenye vigezo na kujua tabia zao hasa katika ufanisi wa kazi zao uwanjani basi lazima kocha wa timu ya Taifa awe na ushirikiakno wa kweli na makocha wa ndani. Kwa mfano kufeli kwa Serengeti boys tutamlaumu Milambo na kwa kiasi fulani anahusika na ushiriki wa aibu wa vijana wale ila Amunike nae kama Kocha mkuu wa timu ya Taifa huwezi kumtoa kwenye lawama za Serengeti boys kufanya vibaya.Mwalimu mkuu wa shule ikiwa moja ya darasa lake limefanya vibaya huwezi kusema hahusiki. Kwa kiasi fulani watanzania bado hatujapata wasimamizi sahihi wa mpira wetu na hicho ndicho kitu kikubwa kinachoitafuna soka letu .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic