April 25, 2019



FT: KMC 1-2 Simba
Wafungaji wa leo kwa upande wa Simba Emmanuel Okwi na John Bocco.

Kwa upande wa KMC ni Hassan Kabunda. 

Dakika 90 za kipindi cha pili zinakamilika zinaongezwa dakika nne.

Kipindi cha pili: KMC 1-2 Simba

Uwanja: CCM Kirumba

Kocha msaidizi wa KMC anatolewa nje na mwamuzi Kambuzi Mwamuzi Abdalah Kambuzi anatoa penalti ya pili kwa Simba, dakika ya 

Simba wanapata penalti baada ya Okwi kucheza madhambi, inapigwa na Kagere ambaye anaikosa uwanja wa CCM Kirumba baada ya kushtua na kudakwa na mlinda mlango Jonathan Nahimana.

Bocco Gooooal dakika ya 83 kwa Simba

Hassan Kabunda Goooool dk ya 57 KMC  

Tayari kipindi cha pili kimeanza

Mpira kwa sasa ni Mapumziko

Kipindi cha kwanza dakika 45 zinakamilika zinaongezwa dakika 2.

Dakika ya 23 Goooooal Emanuel Okwi

Njano, Zana Coulibaly anapewa kadi ya njano.

Mabadaliko kwa KMC, Kelvin Kajiri anaingia akichukua nafasi ya Alon Lulambo dk ya 20 ambaye ameumia, George Sangija anakwenda benchi anaingia James Msuva, Sixtus Sabilo anakwenda benchi anaingia Omary Ramadhan

 James Kotei anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Mzamiru Yassin kwa Simba, Okwi anakwenda benchi anaingia Hassan Dilunga, Mohamed Ibrahim anaingia akichukua nafasi ya Chama

 
MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya KMC na Simba  kwa sasa ni kipindi cha pili, uwanja wa CCM Kirumba ambapo wenyeji ni KMC.

KMC wanakumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 2-1.

Okwi anawanyanyua mashabiki wa Simba dakika ya 23 baada ya kuwahadaa mabeki wa KMC wakidhani ameotea.

Kabunda anafunga bao la kusawazisha dakika ya 57.

Mashabiki waliojitokeza leo ni wachache  siku ya leo ambayo ni katikati ya juma hali ambayo imefanya wengi kushindwa kujitokeza kuona namna amshaamsha zilivyo uwanja wa CCM Kirumba.

9 COMMENTS:

  1. Msimamo Wa Wafungaji Okwi Anazidi Kujikongoja Na Goal 10 Mpaka Mapumziko Makambo Na Aiyee Wajipange Wasijekushanga Wa Kwanza Kagere 2 Bocco 3. Okwi 4. Makambo Au Aiyee

    ReplyDelete
  2. Dah! Kagere Na Ka Staili Kake Ka Kila Siku Leo Kame Mponza Leo Ilitakiwa Abadili Mtindo Wake Wa Kupiga Penati

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Unashangaa nini?Kwani ukifanya madhambi matano yanayostahili penalti kwenye penalti box zisitolewe kwa kuwa imetolea moja?
    Kuna sheria inayosema penalti ni moja tu?Ikitolewa basi mchezaji hata akishika haitolewi penalti?

    ReplyDelete
  5. Halafu kuna mjinga huko wa Congo asiyejua hesabu hata kidogo bali kutoa shutuma na kuropoka na kuongea ..anatupigia hesabu namna jangwani Fc itakavyokuwa Bingwa!Hivi wanaanzaje au wanawezaje!

    Zahera soma hiuo....bado ngapi hukoooo na bado viporo vingapi?

    ReplyDelete
  6. Vipi asome nae hajuwi hesabu. Yeye anachokijuwa ni majisifu na kufukuza wachezaji na kufundisha namna ya kuzungusha bakuli. Ati anangoja kusherehekea ubingwa. Atamuweza wapi mnyama

    ReplyDelete
  7. erasto kumpa pasi manula ikawa offside, kweli kunya anye kuku, akinya bata kaharisha, this is simba brother

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic